Sunday, January 25, 2015

PAKACHA

Wazanzibari tumebarikiwa sifa ya kutunza, kulinda na kuendeleza utamaduni wetu. Pakacha ni kitu ambacho hutengezwa kwa kutumia makuti na kazi yake ni kubebea vitu mbali mbali kama machungwa, embe, chenza, kuku na hata kitoweo, hivyo basi naweza kusema pakacha ni aina ya mkoba wa asili ambao umeanza kutumiwa tangu zamani na mababu na mabibi zetu na hadi hii leo bado tunaendeleza asili hiyo ya kutumia dhana hyo. Tudumishe asili na utamaduni wetu wa kizanzibari.

No comments:

Post a Comment