ASILI NA UTAMADUNI WA ZANZIBAR
Monday, January 26, 2015
Sherehe mbali mbali za asili na kiutamaduni
Ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba kuna sherehe mbali mbali za kiutamaduni kama sherehe za mwaka kogwa, fensi, sauti za busara, tamasha la nchi za jahazi na nyenginezo.
Mkoba wa ukili
Mkoba wa ukili hutengenezwa kwa kutumia ukindu, uzi wa ukindu na shazia. Huu ni mkoba wa asili lakini pia unaonesha utamaduni wa watu wa zanzibar.
Sunday, January 25, 2015
VIUNGO VYA ASILI
Ndani ya visiwa vya zanzibar kuna viungo vingi vya asili ambavyo hutumiwa kwa ajili ya kutia katika vyakula kama vile chai na pilau. Pia wakaazi wa visiwa vya zanzibar hutumia viungo hivyo kwa maswala ya urembo na dawa. Viungo hivyo ni kama tangawizi, mdalasini, uzile, hiliki, pilipili manga, manjano na vyenginevyo.
NGOMA ZA ASILI NA UTAMADUNI ZA ZANZIBAR
Visiwa vya zanzibar vimebahatika kuwa na ngoma mbali mbali za asili kama vile msewe, kibati, beni, njugu, mwanandege na nyenginezo nyingi. Ngoma hizo zinapochezwa, wachezaji huvaa mavazi ya asili kama vile seruni, kanga, chachacha za miguuni, ukindu, usinga na hata kuchukua fimbo. Na dhana kama vile ngoma, tarumbeta, cherewa na kadhalika. Tudumishe ngoma zetu za asili zanzibar.
RESI ZA NGARAWA
Resi za ngarawa ni moja kati ya burudani nzuri na za kuvutia za asili na kiutamaduni ambazo hufanyka ndani ya visiwa vya zanzibar.
PAKACHA
Wazanzibari
tumebarikiwa sifa ya kutunza, kulinda na kuendeleza utamaduni wetu.
Pakacha ni kitu ambacho hutengezwa kwa kutumia makuti na kazi yake ni
kubebea vitu mbali mbali kama machungwa, embe, chenza, kuku na hata
kitoweo, hivyo basi naweza kusema pakacha ni aina ya mkoba wa asili
ambao umeanza kutumiwa tangu zamani na mababu na mabibi zetu na hadi hii
leo bado tunaendeleza asili hiyo ya kutumia dhana hyo. Tudumishe asili
na utamaduni wetu wa kizanzibari.
BAIBUI LA KAMBA NA NIKABU
Baibui la kamba ni vazi la zamani linaloonesha utamaduni wa watu wa zanzibar ambalo huvaliwa na wanawake wa zanzibar wanapokwenda safarini na hata harusini. pia kwa hapo zamani maharusi walikuwa wakivishwa vazi hili. Na nikabu ni kivazi kinachoziba uso na kubakisha macho tu, nayo pia inaonesha utamaduni wa wanawake wa kizanzibari. Kiujumla hayo ni mavazi yanayopendeza sana na yanayowasitiri vizuri wanawake. Tudumishe utamaduni.
Subscribe to:
Posts (Atom)